Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amesisitiza kuwa dhamira yake ni kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza akiwa na Manchester United baada ya kupona majeraha.
Ibrahimovic 36, alikuwa nje ya uwanja tangu mwezi April mwaka huu akifunga mabao 28 katika michezo 46 msimu uliopita.
Akiwa anaendelea kuuguza majeraha yake ambayo yalitarajiwa yangemuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu zaidi United ilimuongezea mkataba wa mwaka mmoja mwezi Agosti mwaka huu.
"Nimerejea kumalizia kazi niliyoianza," Ibrahimovic alimwambia mchambuzi wa Sky Sports wakati akizungumzia mechi ya kesho ya United dhidi ya Tottenham Hotspur.
"Kama nilivyosema nimerejea kumalizia kazi niliyoianza, msimu uliopita tulishinda mataji matatu lakini ndoto yangu ni kutwaa ligi kuu ya Uingereza.
Raia huyo wa Sweden aliiwezesha United kushinda ngao ya jamii, kombe la ligi na taji la Europa lililoifanya kupata nafasi ya kushiriki ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu huu.
IBRAHIMOVIC: NIMEREJEA KUIPA UBINGWA UNITED
Title: IBRAHIMOVIC: NIMEREJEA KUIPA UBINGWA UNITED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji Zlatan Ibrahimovic amesisitiza kuwa dhamira yake ni kutwaa taji la ligi kuu nchini Uingereza akiwa na Manchester United baada...
Post a Comment