Samata amekuwa akiisaidia Genk kufanya vizuri hata asipofanikiwa kufunga bao anaonyesha uwezo na kusaidia wenzie kufunga.
Katika mchezo wa juzi Jumatano walioibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Club Brugge, Samata alifunga bao la pili dakika ya 90 kwa shuti kali hali iliyoamsha shangwe uwanja mzima.
Mashabiki wa Genk walionyesha bango la nahodha huyo akiwa na jezi ya Stars ikiwa ndani ya bendera ya Tanzania na kuitangaza nchini huko Ubelgiji.
Genk iko nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 17 alama 13 nyuma ya vinara Brugge.
UKIWA UWANJANI MTU HUWA NA FARAJA SANA ASA PALE UNAPOONA TANZANIA INAPOTANGAZWA NA KUJULIKANA.
ReplyDelete