Ancelotti anahusishwa na kuchukua kibarua ndani ya Goodison Park baada ya Ronald Koeman kutimuliwa baada ya michezo tisa msimu huu.
Raia huyo Italia, alitupiwa virago na Bayern Munich mwezi Septemba ni miongoni mwa makocha wenye majina makubwa akiwa tayari ametwaa mataji matatu ya klabu bingwa Ulaya, ubingwa wa ligi katika nchi za Uingereza, Italia, Ufaransa na Ujerumani.
Pamoja na mafanikio hayo, Pearce anaamini Ancelotti akijiunga na Everton hakutakuwa na tofauti na mameneja wengine katika ligi barani Ulaya.
"Rafa Benitez yupo ni Newcastle na inaweza isiwe tofauti na suala hili la Anchelloti. Unaweza ukajiuliza kwanini Rafa ameshinda ligi ya mabingwa Ulaya lakini yupo Newcastle?
"Naweza kusema Everton ni klabu kubwa, inacheza ligi kuu Uingereza pia haina matatizo ya kifedha, hakuna meneja katika dunia ya soka ambaye anasema Everton ni klabu ndogo na hawezi kuifundisha," alisema Pearce
LABDA ANAWEZA AKAWA MSAADA AISEE!
ReplyDelete