SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: OKWI AJIB WABANWA MECHI YAISHA PACHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nyota Emmanuel Okwi wa Simba na Ibrahim wa Yanga wameshindwa kufurukuta na kufunga katika mchezo wa watani wa jadi uliomalizika kwa sare y...
Nyota Emmanuel Okwi wa Simba na Ibrahim wa Yanga wameshindwa kufurukuta na kufunga katika mchezo wa watani wa jadi uliomalizika kwa sare ya bao moja uliofanyika kwenye uwanja wa Uhuru.

Wachezaji hao walikuwa wakipewa nafasi kubwa ya kufunga kwenye mchezo huo kutokana na viwango vyao kwa sasa lakini waliweza kudhibitiwa na kuondoka uwanjani bila kuziona nyavu.

Simba ilianza kwa kasi mchezo huo ambapo ilifanya mashambulizi kadhaa langoni mwa Yanga lakini yaliishia kwa mabeki Kelvin Yondan na Andrew Vincent 'Dante'.

Kiungo Papy Tshishimbi alifanya kazi kubwa kutibua mipango ya Simba kuanzia katikati ya uwanja na kufanikiwa kupiga mashuti mawili kipindi cha kwanza yaliyopanguliwa na mlinda mlango Aishi Manula.

Shiza Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza dakika ya 57 baada ya kutokea piga nikupige langoni mwa Yanga lililodumu kwa dakika tatu tu baada ya Obrey Chirwa kusawazisha akimalizia krosi ya Geofrey Mwashiuya.

Kocha wa Yanga George Lwamina aliwapumzisha Raphael Daud na Mwashiuya na kuwaingiza Emmanuel Martin na Pato Ngonyani.

Kwa upande wa Joseph Omog aliwaingiza Jonas Mkude na Said Ndemla kuchukua nafasi za James Kotei na Mzamiru Yassin.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top