Rais wa Shirikisho la Mpira
wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia ameunda Kamati ya Tuzo za Ligi Kuu ya
Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2017/18.
Kamati hiyo itaongozwa na Mwenyekiti Ahmed
Mgoyi wakati Makamu Mwenyekiti ni Almas Kasongo ilihali Amiri Mhando
ameteuliwa kuwa Katibu wa kamati hiyo ya tuzo.
Mhando ni Mhariri wa Gazeti la Spotileo
linalotolewa na Kampuni ya Magazeti ya Serikali - Tanzania Standard Newspaper
(TSN).
Wajumbe ambao wameteuliwa ni Ibrahim Kaude;
Mkuu wa Kitengo cha Michezo katika Kampuni ya Azam Media, Patrick Kahemele na
Kocha mkongwe wa soka, Kenny ‘Mzazi’ Mwaisabula.
Kadhaika Mhariri Mtendaji wa Kampuni ya
Uchapishaji ya Global (Global Publisher inayochapisha magazeti kadhaa likiwamo
Championi), Saleh Ally; Mtangazaji mahiri wa michezo kutoka Kituo cha Redio cha
EFM, Ibrahim Masoud na Mtangazaji wa Vipindi katika Kituo cha Radio ya Watu,
Fatma Likwata.
Pia wamo Mwandishi Mwandamizi wa Michezo wa
Gazeti la Mwanaspoti linalochapishwa na Kampuni ya Mwananchi Communication
(MCL), Gift Macha; Katibu Mkuu wa Chama cha Wachezaji wa Mpira wa Miguu, Said
George na Mhariri wa Michezo wa Gazeti la HabariLeo linalotolewa na TSN, Zena
Chande.
Post a Comment