Shirikisho la Mpira wa Miguu
Tanzania linapenda kuwatangazia wananchi kuwa viingilio katika mchezo wa Ligi
Kuu ya Vodacom Tanzania Bara kati ya Azam na Simba.
Mchezo huo utafanyika Uwanja wa Azam ulioko
Chamazi, Dar es Salaam na viingilio vitakuwa shilingi elfu kumi (Sh 10,000) kwa
Jukwaa Kuu ambalo lina uwezo wa kubeba mashabiki 1,000 tu walioketi, wakati
mzunguko (popular) kiingilio kitakuwa ni shilingi elfu saba tu (Sh 7,000).
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania
linapenda kuwatangazia wanafamilia ya mpira wa miguu kukata tiketi kuanzia leo
Jumatano Septemba 6, mwaka huu ili kujiepusha na usumbufu wa aina yoyote.
Kadhalika tunapenda
kuwatangazia wananchi kwamba kwa ye yote ambaye hana tiketi ni vema wasiende
uwanjani kwani ujio wake hautakuwa na tafasiri nyingine zaidi ya kuonekana kuwa
ni mleta fujo.
Vyombo vya usalama vitakuwa
makini kudhibniti kila aina ya vurugu uwanjani hapo hasa ikizingatiwa kuwa mchezo
huo utafanyika wakati jua limezama. Mchezo utakuwa Septemba 9, 2017 saa 1.00
(19h00).
Post a Comment