Ligi Kuu ya Vodacom
Tanzania Bara (VPL) inatarajiwa kuendelea kesho Jumamosi Septemba 23, mwaka huu
kwa michezo mitatu kuchezwa katika viwanja tofauti hapa nchini.
Kesho Jumamosi Young
Africans itacheza na Ndanda FC ya Mtwara kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam
wakati Tanzania Prisons itakuwa mgeni wa Mwadui ya Shinyanga katika mchezo
utaofanyika Uwanja wa Mwadui.
Mchezo mwingine,
utakutanisha timu za Majimaji itakayokuwa mwenyeji wa Njombe Mji kwenye Uwanja
wa Majimaji mjini Songea. Mechi zote hizo zitaanza saa 10.00 jioni.


Post a Comment