Timu ya soka ya Simba imeshindwa kuendelea wimbi la
ushindi baada ya kulazimishwa sare timu ya Mbao fc ya bao 2-2 katika uwanja wa
Ccm Kirumba Jijini Mwanza
Simba walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa
winga wake Shiza Kichuya mapema katika dakika ya 16 baada ya kuunganisha vyema
krosi ya Erasto Nyoni, mpaka mapumziko Simba walikuwa mbele kwa bao 1-0
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na Mbao
kusawazisha kupitia kwa Habibi kiyombo katika dakika ya 46, Simba walicharuka
iliwachukua dakika mbili James Kotei akaipatia Simba goli la pili.
Zikiwa zimesalia dakika 10 beki Boniface Maganga
alisawazishia Mbao kwa goli zuri kabisa katika dakika ya 81 kwa kuupiga mpira
uliomshinda Kipa Manua mpaka dakika 90 Mbao 2-2 Simba
Simba walifanya mabadiliko kwa kuwatoa Shiza Kichuya
na Asamoah Gyan nafasi zao zikachukuliwa na Haruna Niyonzima na Juma Luizio
Simba wamefikisha Pointi 8 baada ya kushinda 2 na
kusuluhu 2, Mechi ijayo Simba atakuwa Shinyanga dhidi ya Stand United siku ya
tarehe 1 oktoba


Post a Comment