Ligi Daraja la Pili Tanzania
Bara (SDL), inatarajiwa kuanza Septemba 30, mwaka huu kwa timu kuchuana katika
viwanja vitano tofauti.
Kwa mujibu wa Ratiba ambayo imeambatanishwa,
michezo ya siku hiyo itakuwa ni kati ya Abajalo na Cosmopolitan; Namungo na
Reha kutoka Kundi A wakati kundi B kutakuwa na mchezo kati ya Pepsi na Madini.
Kundi C kutakuwa na mchezo kati ya Burkinafaso
na Ihefu kadhalika Boma itacheza na Mkamba Rangers huku Kundi D likikutanisha
timu za Bulyanhulu na Milambo.
Katika Kundi hilo la D Mchezo kati ya Nyanza
FC na Area C uliokuwa ufanyike Septemba 30, 2017 siku ya Jumamosi kwenye Uwanja
wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, sasa utachezwa Oktoba 01, 2017 siku ya
Jumapili kwenye Uwanja huo huo.
Sababu za mabadiliko haya ni kutokana na
mchezo kati ya Pepsi FC vs Madini FC kuchezwa tarehe 30.09.2017 katika uwanja huo.
Awali mchezo wa Nyanza na Area C ulipangwa kufanyika mkoani Manyara, lakini
kutokana na hali ya uwanja ilibidi Bodi ya ligi ufanye mabadiliko husika.


Post a Comment