Uongozi wa klabu ya Simba bado una imani na kocha Joseph Omog na hawajampa mechi yoyote ili wamtimue.
Kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abdallah 'Try Again' alikutana na kocha huyo raia wa Cameroon jana baada ya kumalizika kwa mchezo dhidi ya Mwadui FC na kumuhakikishia nafasi bado ipo ndani ya Wekundu hao.
Msemaji wa timu hiyo Hajji Manara amewaambia Waandishi kuwa Mashabiki wanamekuwa wakimpigia kelele kocha huyo ila Uongozi hauko tayari kumuacha kocha huyo.
"Mashabiki wa Simba sijui wanataka nini timu inafanya vizuri lakini hawamtaki kocha.
"Simba imecheza mechi tisa bila kufungwa hata bao moja lakini kwa sasa kila mtu anajifanya kocha ila Omog haondoki," alisema Manara.
Manara alisema kikosi kamili cha Simba kitaondoka Kesho kuelekea jijini Mwanza kwa ajili ya mchezo dhidi ya Mbao siku ya Alhamisi.
SIMBA: OMOG NI WA HAPA HAPA HAONDOKI NG'O
Title: SIMBA: OMOG NI WA HAPA HAPA HAONDOKI NG'O
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uongozi wa klabu ya Simba bado una imani na kocha Joseph Omog na hawajampa mechi yoyote ili wamtimue. Kaimu Rais wa klabu hiyo Salim Abd...


Post a Comment