Mzunguko wa Tatu wa Ligi Kuu
ya Vodacom Tanzania Bara (VPL), inatarajiwa kuendelea leo na wikiendi yote
Azam FC itaialika Kagera
Sugar saa 1.00 usiku (19h00) katika Uwanja wa Azam ulioko Chamazi jijini Dar es
salaam.
Kesho Jumamosi Mabingwa watetezi Young Africans mgeni wa Majimaji FC ya Songea saa
10.00 jioni (16h00) katika Uwanja wa Majimaji mkoani Ruvuma.
Mbao itasafiri hadi Manungu mkoani Morogoro
kucheza na Mtibwa Sugar katika mchezo ambao pia utapigwa Jumamosi saa 16h00
wakati Tanzania Prisons ya Mbeya itakuwa mwenyeji wa Ndanda FC saa 16h00 kwenye
Uwanja wa Sokoine.
Lipuli Fc itakuwa mwenyeji wa Ruvu Shooting
saa 16h00 katika Uwanja wa Samora, Iringa wakati Stand United itacheza na
Singida United saa 16h00 kwenye Uwanja wa Kambarage, Shinyanga.
Siku ya Jumapili Septemba 17, 2017 Mbeya City
itaikaribisha Njombe Mji saa 16h00 kwenye Uwanja wa Sokoine jijini Mbeya huku
Simba SC ikiwa mwenyeji wa Mwadui FC saa 16h00 jioni katika Uwanja wa Uhuru,
Dar es salaam.

Post a Comment