Kiungo mkabaji wa zamani wa Manchester united Roy keane,ameziponda timu kongwe na zenye mafanikio kwa soka la uingereza Liverpool.na Manchester kwa kupigania au kushangilia kuingia top four badala ya kupigania kutwaa ubingwa,Keane ambae pia alikuwa moja ya manahodha wenye mafanikio kwa Manchester united amesema ni aibu kubwa sana kwa timu za aina ya Liverpool au Manchester united kushangilia kuingia top four badala ya kupigania ubingwa,hivi toka lini ukaona real Madrid au Barcelona wanashangilia kuingia top four? Alihoji Keane,mbali hilo Keane pia amesema timu hizo zimeshindwa hata kuikaibia Tottenham Hotspurs huku pia wakiiacha Chelsea akitawala kileleni kwa muda mrefu.
Katika hali inavyoonekana Manchester itatakiwa kushinda ubingwa wa uefa ndogo ili kujihakikishia nafasi ya kushiriki ubingwa wa vilabu bingwa ulaya msimu ujao,huku liverpool ikitakiwa kuhakikisha inashinda mechi zake zilizobaki ili kubaki katika nafasi iliyopo.
Ninapoona timu hizi zinashangilia kuingia top four nahisi aibu kubwa sana,alimalizia Keane.
ROY KEANE AZIPONDA LIVERPOOL NA MANCHESTER UNITED
Title: ROY KEANE AZIPONDA LIVERPOOL NA MANCHESTER UNITED
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kiungo mkabaji wa zamani wa Manchester united Roy keane,ameziponda timu kongwe na zenye mafanikio kwa soka la uingereza Liverpool.na Manch...
Kila mtume na zama zake,zama za hao watani zimepita,wanapaswa kujipanga upya kurudi
ReplyDelete