Baada ya Jana kuenea kwa taarifa iliyoripotiwa
kuwekwa na Rais wa TFF Jamal malinzi juu ya kufanya droo ya kujua uwanja gani
utatumika kwa fainali ya kombe hilo baina ya Simba na Mbao,hatimaye Leo TFF
imekata mzizi wa fitna baada ya kutangaza kwamba mechi hiyo itapigwa dodoma
tarehe 28/05/2017.
Mashabiki wengi wa soka nchini walionekana
kushtushwa na taarifa aliyotoa malinzi kupitia mtandao wake wa Twitter juu ya
kufanyika kwa droo hiyo ambapo walisema hakuna utaratibu kama huo
duniani,lakini wakati mashabiki wa soka wakisubiri kuona kufanyika kwa droo
hiyo ghafla taarifa ikatolewa na TFF Leo hii kwamba mechi hiyo itafanyika Mjini
Dodoma.
Simba na mbao zilingia fainali baada ya kuzifunga
azam na yanga kwa goli 1-0,hivyo kuzifanya timu hizo kukutana kuamua nani
atawakilisha nchi kwenye kombe la shirikisho barani Africa mwakani.
Mbao imeweka historia kuwa timu iliyopanda daraja na
kuja kufanya makubwa katika soka.la Tanzania kwa kuweza kuvitingisha vigogo
kama.simba,yanga,azam,mtibwa sugar nk
Post a Comment