SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA: MOTO UTAWAKA SIMBA AKIPEWA POINTI ZA MEZANI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Salum Mkemi kulia Mjumbe wa kamati ya utenda ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi ameionya Bodi ya ligi isithubutu kuwapa pointi za mezani tim...
Salum Mkemi kulia
Mjumbe wa kamati ya utenda ya klabu ya Yanga, Salum Mkemi ameionya Bodi ya ligi isithubutu kuwapa pointi za mezani timu ya Simba. Timu ya Simba imemkatia rufaa beki wa Kagera Suger Mohamed Fakh ikieleza kuwa mchezaji huyo alichezeshwa akiwa na kadi tatu za njano kinyume na kanuni za ligi.

Mkemi amesema kuwa Yanga wana maslahi makubwa katika sakata hilo kwa kuwa wanapigania ubingwa hivyo hawataweza kukaa kimya.

Mkemi amesema kamati ya utendaji ya Yanga imekaa jana na imeafikiana kwamba hawatakubali Simba wapewe pointi za mezani kwa kuwa rufaa yao ina mapungufu.

"Tuko tayari kuwabeba Kagera mgongoni kwa garama yoyote mpaka haki yao ipatikane kwa sababu hizo pointi zina maslahi yetu kwa kuwa tunahitaji kutetea ubingwa wetu."

Mkemi alisema Fakhi alionyeshwa kadi kwenye michezo miwili ya ligi na mmoja wa FA kwahiyo kanuni hazikuvunjwa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Kwa hali hii inabidi tushinde mechi zote zilizobaki ...... kila la heri mnyama

    ReplyDelete

 
Top