Wekundu wa Msimbazi Simba Sc leo wamefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa magoli 3 - 2 ugenini dhidi ya Mbao fc katika dimba la CCM Kirumba Jijini Mwanza.
Mbao itabidi wajilaumu wenyewe baada ya kutangulia kwa magoli 2 yote yakipatikana kipindi cha kwanza kupitia kwa George Sagia dakiya ya 20 na la pili likifungwa na Evangerusts Bernard dakika ya 33 wakitumia udhaifu wa beki za kati za Simba Juuko Murushid na Basela Bukungu ambao walikua hawana maelewano mazuri.
Kabla timu hazijaenda mapumziko kocha wa Simba aliona mapungufu ya timu yake katikati na kwenye ushambuliaji ambapo.ilimlazimu kufanya mabadiliko kwa kumtoa Pastory Athanas na Hamadi Juma akawaingiza Saidi Hamis Ndemla na Laudit Mavugo mabadiliko ambayo yaliweza kutuliza Timu kwa kiwango kikubwa.
Mpaka timu zinaenda mapumziko Mbao fc walikua wanaongoza goli 2 kwa bila.
Kipindi chapili simba walikuja kwa kasi na kulishambulia lango la Mbao mfululizo lakini washambuliaji wake hawakua makini.
Mshambuliaji Fredrick Blagnon aliingia kuchukua nafasi ya Juma Luizio aliwanyanyua mashabiki wa simba waliokua wanyonge uwanjani dakika ya 82 kwa kuiandikia Simba goli la kwanza goli ambalo lilirudisha uhai na dakika ya 90 Blagnon tena akawarudisha mashabiki waliokua wameshatoka uwanjani kwa kufunga goli la pili,Lakini pia kama miujiza dakika za nyongeza mwishoni kabisa ikatokea piga nikupige langoni kwa Mbao ambapo beki mmoja wa mbao aliokoa vibaya kwa kichwa na mpira kumkuta Mzamiru Yasin akapiga shuti kali na kuiandikia timu yake goli la 3
Mpaka Mwamuzi anapuliza filimbi kuishiria mpira umekwisha simba 3 Mbao 2.
Kwamatokeo hayo simba imepanda kileleni kwakufikisha pointi 58 ikiwa imeshuka dimbani mechi 26.
Simba itashuka tena katika uwanja huo wa kirumba siku ya jumamosi kucheza na Toto African na hiyo itakuwa mechi yao ya mwisho katika kanda ya ziwa msimu huu.
Matokeo mengine leo huko Manungu Azam fc imelazimisha sare ya bila kufungana na Mtibwa Sugar
SIMBA WARUDI KILELENI LIGI KUU
Title: SIMBA WARUDI KILELENI LIGI KUU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Wekundu wa Msimbazi Simba Sc leo wamefufua matumaini ya kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania Bara baada ya kupata ushindi wa magoli 3 - 2 u...
Post a Comment