YANGA KUWAFUATA WAARABU KESHO
Klabu ya soka ya Yanga SC itakwea pipa hapo kesho kuelekea Algeria katika mechi ya marudiano dhidi ya Mc Alger
Msafara wa wachezaji 20, benchi la ufundi na viongozi utaondoka kesho jioni majira ya saa 12 kwa ndege ya shirika la ndege la Emirates kupitia Dubai.
Wachezaji watakaondoka ni Makipa; Deogratius Munishi na Beno Kakolanya. Nafasi ya ulinzi ni; Nadir Haroub , Vicent Bossou , Juma Abdul , Vicent Andrew, Oscar Joshua , Juma Abdul , Mwinyi Haji, Hassan Kessy na Kelvin Yondani.
Nafasi ya viungo ni; Thabani Kamusoko, Haruna Niyonzima, Deus Kaseke, Said Makapu, Juma Mahadhi, Saimon Msuva, Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin.
Upande wa washambuliaji ni Amis Tambwe na Donald Ngoma
Wachezaji watakaokosa mchezo huo kwa sababu mbalimbali ni Justine Zulu, Malimi Busungu, Matheo Antony, Ally Mustapha, Pato Ngonyani, Obrey Chirwa na Yusuph
Yanga inaenda Algeria kutafuta ushindi au sare ya aina yoyote baada ya kupata ushindi wa goli moja kwenye mchezo wa awali uliofanyika Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.
Post a Comment