SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: UCHAGUZI DRFA WAFANYIKA SALAMA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Almas Kasongo ameendelea kutetea nafasi ya uenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)  kwa kuibuka na kura 12 dhidi kura 9 ...

Almas Kasongo ameendelea kutetea nafasi ya uenyekiti wa chama cha soka mkoa wa Dar es Salaam (DRFA)  kwa kuibuka na kura 12 dhidi kura 9 za mpinzani wake wakaribu Peter Muh

Katika uchaguzi huo Salum Mwaking'anda ameshinda nafasi ya  makamu mwenyekiti huku nafasi ya katibu akichukua Msanifu Kondo.

Akizungumza baada ya matokeo ya uchaguzi huo Kasongo aliwashukuru wajumbe wa kamati ya utenda kwa imani kubwa waliyonayo juu yake kwa kumchagua tena kwa awamu ya pili na kuahidi kuleta maendeleo ya soka la Dar es Salaam.

"Nawashukuru wajumbe kwa kuonyesha imani kubwa kwangu na ninaahidi katika miaka minne mingine kwa kushirikiana na wenzangu tutaendelea kuinua soka la Dar," alisema Kasongo.

Shaffih Dauda amechaguliwa kuwa mjumbe mwakilishi wa vilabu huku Amour Amour, Bakari Mtumwa na Funua Ally wakichaguliwa kwenye kamati ya utendaji.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top