SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: WAZIRI DK. MWAKYEMBE AKABIDHI BENDERA SERENGETI BOYS, AHAMASISHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe  (Mb) leo tarehe 3 Aprili 2017 ameshiriki kwenye zoezi la ...
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe  (Mb) leo tarehe 3 Aprili 2017 ameshiriki kwenye zoezi la kuwaaga na kuwapatia bendera ya Taifa timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri chini ya miaka 17 (Serengeti Boys).

Mhe. Mwakyembe amewaasa vijana wa Serengeti kuliwakilisha vyema Taifa kwenye michuano ya AFCON wanayotarajia kwenda kushiriki hivi karibuni.

Mhe. Mwakyembe akiongozana na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Bw. Jamal Malinzi aliwahakikishia vijana wa Serengeti utayari wa Serikali katika kuendeleza mpira wa miguu nchini.

Vilevile, Mhe. Mwakyembe ametoa rai kwa Watanzania kuendelea kuwachangia Serengeti Boys ili waweze kuwa na ushiriki bora katika michezo ya maandalizi nchini Morroco na Cameroun na baadaye katika michuano ya AFCON, nchini Gabon.

Sambamba na hilo Mhe. Mwakyembe aliwaongoza wananchi waliofika uwanja wa Taifa kuishangilia Serengeti boys iliyokuwa ikicheza mechi ya kirafiki na timu ya Taifa ya vijana kutoka Ghana, ambapo Serengeti boys wameweza kurudisha magoli mawili na matokeo hadi mwisho yakawa sare ya 2-2.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top