KUZIONA YANGA NA MC ALGER BUKU 5 TU
Timu ya soka ya Mc Alger ya Algeria inatarajiwa kuingia nchini siku ya alhamisi kwaajili ya mchezo wakombe la shirikisho dhidi ya wenyeji wao Yanga ssc utakao chezwa kwenye uwanja wa taifa Dar es salaam siku ya jumamosi saa kumi jioni.
Akiongea na waandishi wahabari leo Katibu mkuu wa yanga Charles Bonifas Mkwasa alisema Timu hiyo ya Algeria itaingia alhamis Saa 3:30 usiku kwa ndege maalum na wataondoka jumamosi baada ya mechi saa tano usiku.
"Tumepata taarifa kwamba Timu ya Mc Alger itawasili tarehe sita siku ya alhamis saa 3:30 kwandege maalum. Sisi kama wenyeji wao tumefanya kila tunachotakiwa kufanya kama Timu mwenyeji lakini kama mnavyojua wenzetu nao wana ubalozi wao hapa wanafanya mambo yao kwakushirikiana nao kwaukaribu".alisema
Katika hatua nyingine Mkwasa ametaja viingilio vya mchezo huo kama ifuatavyo Mzunguko wote 5000, v.i.p B na C itakua 20,000 na v.i.p A sh 30,000.
Vile vile Katibu huyo mwenye taaluma ya ukocha amewaomba wanachama na mashabiki wa Timu hiyo wajitokeze kwa wingi uwanjani siku ya jumamosi ili waweze kuisapoti timu yao.
Pia Mkwasa amekanusha taarifa zinazoenea kwenye mitandao na baadhi ya vyombo vya habari kwamba Klabu ya Yanga inampango wa kuachana na kocha wao George Lwandamina na kumchukua kocha wa zamani wa Azam Stewart Hall.
"Kuna taarifa zinaenenea kwenye mitandao ya kijamii na baadhi ya vyombo vya habari kwamba tuna mpango wakuachana na kocha wetu Lwandamina na kuleta kocha mwingine sio zakweli, taarifa za yanga zinatolewa na mimi au uongozi wa Yanga waandishi mkiona taarifa ambayo hamna uhakika nayo Simu zetu ziko wazi na ofisi zetu pia".alisema
Post a Comment