SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SERENGETI WAWAAGA WATANZANIA KWA SARE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys U17 imelazimishwa sare ya magoli 2. 2 na Timu vijana ya Ghana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa ...
Timu ya Taifa ya vijana Serengeti Boys U17 imelazimishwa sare ya magoli 2. 2 na Timu vijana ya Ghana katika mchezo wa kirafiki uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa.

Mechi hiyo ilikua maalum kwaajili ya kuwaaga vijana hao na kukabidhiwa bendera na Waziri wa michezo Dk Harson Mwakiyembe Tukio ambalo lilifanyika kabla ya mchezo haujaanza.

Vijana wa Ghana walimiliki mpira haswa kipindi cha kwanza walipata magoli yao kipindi cha kwanza na chapili kupitia kwa Sulley Ibrahim dakika ya 21baada ya uzembe uliofanywa na mabeki wa serengeti kutokumkaba mpaka akapiga shuti Arko Mensah aliipatia timu yake goli la pili.

Vijana wa Serengeti walifanya kazi ya ziada kwakulishambulia lango la wapinzani wao kama nyuki na dakika ya 90 walipata penalti baada ya beki wa vijana wa ghana kunawa mpira ndani ya penalti na mwamuzi Elly Sasii akaamuru penalti ambayo ilipigwa kwa ufundi mkubwa na Assad Juma vijana hawakukata tamaa na dakika za nyongeza Muhsin Malima aliweza kuwanyanyua watanzania baada ya kupokea krosi ya Said Mussa.


Kocha wa Serengeti aliwatoa Shabani Zuber na Abdallah Rashid na kuwaingiza Muhsin Malima na Said Mussa kwaupande wa Ghana waliwatoa Yakubu Najeeb, Alhasan Rashid,owusu Bismark Terry nafasi zao wakaingia Acouah Gideon, Arko  Mensah na Iddriss Mohamed.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top