SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YACHINJIWA BAHARINI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ilokutana Leo  Jumanne kwa lengo la kupiti...
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), ilokutana Leo  Jumanne kwa lengo la kupitia uamuzi uliofanywa na Kamati ya Usimamizi na Uendeshaji Ligi Tanzania maarufu kwa jina la Kamati ya Saa 72,imeichinjia baharini klabu ya Simba baada ya kuipokonya tena point zake 3 na magoli matatu walopewa na kamati ya masaa 72 na kuzirudisha kwa kagera sugar.

Kwa mujibu wa Katiba ya TFF, Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji ya TFF, ina mamlaka ya kutafsiri sheria na kanuni za mpira wa miguu nchini kama ilivyoainishwa kwenye katiba na sehemu ya utangulizi ya kanuni za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

Katika mchezo huo, Kagera Sugar ilishinda mabao 2-1, lakini Simba ilikata rufaa ikidai kuwa Kagera Sugar ilivunja kanuni ya 37 (4) ya Ligi Kuu ya Vodacom kwa kumchezesha mchezaji Fakhi Mohammed ambaye alidaiwa na Simba kuwa alikuwa na kadi tatu za njano katika mechi tofauti za Liku Kuu ya Vodacom. Hivyo, ikaadhibiwa kwa mujibu wa kanuni ya 37 (37) ambayo ilitoa pointi tatu na magoli matatu kwa Simba.

Sababu za kurudishwa pointi 3 kwa Kagera Sugar ni
1. Simba hawakuwasilisha madai yao kwa wakati sahihi.
2. Malalamiko ya Simba hayakulipiwa ada kwa mujibu wa kanuni kiasi cha Shilingi laki 3.
3. Kikao cha kamati ya Masaa 72 ilikosa uhalali baada ya kuwashirikisha watu ambao hawakupaswa kuwepo kikaoni.

Sambamba na adhabu hizo mbili kwa Simba lakini baadhi ya watendaji wa ligi wamepelekwa kwenye kamati ya nidhamu baada ya kuipotosha kamati ya saa 72.


Kwa maamuzi hayo ya Leo,ina maana kuwa Simba imebakiwa na point 59 point 3 mbele ya mahasimu wake yanga lakini wakiwa wameizidi yanga kwa michezo miwili kitu ambacho ni kama.kimeweka matumaini ya timu hiyo ya msimbazi ambayo imekaa miaka minne bila ya kutwaa ubingwa wa bara kuwa finyu.


About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top