SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA YAIFATA SIMBA NA AZAM NUSU FAINALI FA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Yanga Africa watoto wa Jangwani wameingia nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuifunga Timu ya Prisons ya Mbeya goli 3. 0...
Timu ya soka ya Yanga Africa watoto wa Jangwani wameingia nusu fainali ya kombe la FA baada ya kuifunga Timu ya Prisons ya Mbeya goli 3. 0 kwenye mchezo wa robo fainali uliochezwa kwenye uwanja wa Taifa Dar es salaam

Mechi hiyo iliyochezwa huku mvua ikiendelea kunyesha ilikuawachukua yanga dakika15 kupata goli lao lakwanza baada Hamisi Tambwe kuunganisha kwa kichwa mpira wa kona iliyo pigwa na Geofrey Mwashiuya na dakika ya    40 Obrey Chirwa akaindikia Timu yake goli pili kwa kichwa tena akiunganisha krosi ya Haji mwinyi, mpaka tim zinaenda mapumziko Yanga walikua mbele kwa magoli mawili.

Kipindi cha pili yanga walirudi kwa kasi na dakika ya 47 Saimon Msuva aliindikia Timu yake goli la 3 kwa shuti kali akiwa nje ya 18, Dakika ya 55 Prison walipata penalti wakashindwa kuitumia vema baada ya Vicktor Hagaya kupiga shuti likagonga mtamba wa panya na kurudi uwanjani mabeki wa Yanga wakaokoa.

Refarii aliwazawadia kadi za njano Nadir Harubu na Hassan Kessy kwa kucheza rafu mbaya upande wa Yanga Huku Mohamedi Samata wa Prisons nae akilimwa kadi kwa mchezo mbaya

Kocha wa Yanga alimtoa Hamis Tambwe na Obrey Chirwa nafasi zao wakaingia Emanuel Martin na Mateo Anton Huku kocha wa Prison akiwatoa Jeremia Juma, Andrew Ntala na Fredy Chudu na kuwaingiza Meshaki Seleman, Aron Kalambo na Victor Hagaya.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top