Bongo kuna nyimbo ya mkongwe wa bongo flavor anaefahamika kama professor Jay au Joseph Haule inaitwa Show ya Kibabe,nadhani ni jina sahihi linaloweza kuielezea wiki hii ilomalizika maana kulifanyika mambo ya kibabe ndani na nje ya viwanja vya michezo.
Tiririka chini hapa uone ubabe wenyewe.
Tanzania
Inawezekana ikawa kuna mengi yametokea lakini kubwa
zaidi ilikuwa ni sakata la rufaa ya klabu ya Simba iliyokubaliwa na kamati
inayosimamia ligi kuu Tanzania almaarufu kama kamati ya masaa 72,lakini kamati
ya katiba sheria na hadhi za wachezaji ikaingilia kati na kuitisha kikao cha
kupitia maamuzi hayo,sakata likachukua sura mpya,kila neno likasemwa hadi
kufikia msemaji wa Simba Haji Manara kuitisha mkutano na wanahabari ili
kuonesha masikitiko ya klabu juu ya muenendeo wa TFF na mambo mbalimbali
yaliyoihusu au yanayoihusu Simba,ebana eeh manara akaongea kibabe,TFF
wakamsikia,wakamtia hatiani na kumpeleka kwenye kamati ya maadili,manara
akajibu kibabe ntaenda kubutua,wakakubaliana jumanne kwa maana kesho aitwe kuhojiwa,unajua
kilichotokea,kamati ikabutua kibabe na kumbutua manara bila kumsikiliza na
kumpiga mvua moja na kubwa kuliko wakampiga na faini la kibabe la mil
9,tunasubiria jibu la kibabe kutoka kwa manara.
Wakati manara anapigwa ban mapema mashabiki wa mpira
kabla hawajakaa sawa wakapokea taarifa nyingine ya kibabe,eeh Simba imepokonywa
point walizopewa na kamati ya masaa 72,wanamsimbazi wakapagawa lakini unajua
kilichowapagawishEti maamuzi ya kamati ya saa 72 hayakuwa sahihi kwa sababu
zifutazo.
1. Simba iliwakilisha rufaa hiyo nje ya muda.
2. Simba haikulipia ada ya kukatia rufaa ambayo ni
pesa madafu kama laki 3.
3. Kali nyingine eti kamati ya saa 72 haikuwa halali
kutoa maamuzi hayo sababu kuna wajumbe walishiriki ambao hawakuwa na haki ya
kushiriki hivyo maamuzi yao yalikuwa batili.
Hahaa yote kwa yote maamuzi haya nayo yalikuwa
yakibabe tu.
Yanga nayo ilitolewa kwenye michezo ya kimataifa
ikaipiga kibabe prison kwenye robo fainali ya kombe la FA maarufu
kama.Azam.confederation cup, kisago cha kibabe cha bao 3-0 kikawatoa prison na
kuipeleka yanga Mwanza kukumbana na Wazee wa mbao,huku game la kibabe la nusu
fainali likipigwa Dsm.kati ya mjeruhiwa wa point Simba dhidi ya waoka mikate wa
azam.
Weekend ya kibabe kwa bongo iliishia kwa mwanariadha
simbu kushika nafasi ya 5 huko kwenye mashindano ya London Marathon,si haba
simbu.
Ah nilitaka kusahau,Serengeti boys ikawabutua kibabe
Gabon ambao ndio wenyeji wa kombe la mataifa ya Africa kwa vijana baadae mwezi
mei kwa bao 2-1 katika mechi ya kirafiki.
Ulaya
Ubabe haukuishia bongo tu,ulaya pia kulikuwa na show
za kibabe,uingereza Chelsea ikaipiga spurs goli 4-2 katika nusu fainali ya
Fa,baada ya hapo arsenal nao wakaibutua man city katika nusu fainali nyingine
ya fa kwa goli za kibabe 2-1,kwahyo fainali itakuwa kati ya wababe wa London,
Chelsea vs Arsenal
Man united ikiwa na kumbukumbu ya kutopata goli
katika uwanja wa turf mor unaomilikiwa na Burnley kwa muda wa miaka 41,iliingia
kibabe na kuifumua Burnley kwa goli 2 -0,
Hatujakaa sawa Huko anfield, wageni crystal palace
waliingia kibabe na kuibutua Liverpool kwa magoli mawili yakikatili yalotiwa
kambani na mshambuliaji wa zamani wa Liverpool Christian benteke,lakini kwa
heshima.kubwa wala hakushangilia,dah soka bana.
Dah unajua show ya.kibabe ya kufungia wiki ilikuwa
wapi....huko Santiago bernabeu,mashabiki elfu 85 walijazana,barca waliingia kwa
unyonge,dah bila neymar maisha yangekuaje,lakini watu wakasahau kwamba kuna
Mfalme mmoja tu ndani ya barca,king messi,akawapiga bao mbili za kibabe huku
ubabe wa Ramos ukimpeleka nje kwa red card,dakika 90,barca 3 Madrid 2,,utamu wa
la liga unazidi kunoga.
Kwa Leo tuishie hapa kwenye weekend yetu ya
kibabe,ila.tumalizie kwa kuhoji,kamati ya katiba na sheria ya TFF kwani
hamkujua Simba hawakukidhi vigezo vya kukata rufaa? Na zile gharama za
kuwalipia nauli viongozi na mchezaji wa kagera na marefariii analipa nani?
Tukutane week ijayo.


Post a Comment