SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: CONTE APAGAWA, MOU JEURI POCHETTINO KICHEKO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Uhondo wa ligi kuu ya uingereza uliendelea Jana baada ya mechi mbili kupigwa,mechi ya kwanza ya mapema.iliwakutanisha Majogoo wa jiji La ...
Uhondo wa ligi kuu ya uingereza uliendelea Jana baada ya mechi mbili kupigwa,mechi ya kwanza ya mapema.iliwakutanisha Majogoo wa jiji La Merseyside, Liverpool.walosafiri kuwafata west Bromwich Albion na kufanikiwa kuibuka na ushindi wa Goli 1-0,shukran kwa bao la mwishoni mwa kipindi cha kwanza kutoka kwa mshambuliaji hatari kutoka Brazil Roberto bobby Firminho aliyeunganisha kwa kichwa mpira wa faulo ilopigwa na James milner,matokeo haya yamewafanya Liverpool kurudi katika nafasi ya 3 baada ya kuipiku Manchester city ilopanda juzi baada ya kuwafunga Southampton kwa magoli 3-0,Liverpool imefikisha point 66 ,point 5 nyuma ya wanaoshika nafasi ya pili Tottenham,na huku wakiwa point 9 nyuma ya vinara Chelsea.

Baada ya mechi hiyo,Dunia ilihamia katika uwanja wa Old Trafford pale vinara Chelsea walipokuwa wageni wa Manchester United ambapo mchezo huo uliisha kwa Chelsea kupokea kichapo cha magoli 2-0 shukrani kwa magoli ya Marcus Rashford na Ande Herera kwenye kila.kipindi,kupoteza kwa mechi kunamfanya Kocha wa Chelsea Antonio Conte kupata mchecheto kwa maana anazidi kupunguza wigo wa Alama kati yao na Tottenham na Liverpool na hivyo kuzifanya mbio za ubingwa msimu huu kuelekea kuwa tamu na ngumu,kwa upande wake,Kocha asietabirika jose mourinho ni kama ushindi huo unazidi kumpa jeuri ya kuwaonyesha.watu kwamba yeye ana uwezo wa kumfunga yeyote pale anapotakiwa kufanya hivyo huku Kocha wa Tottenham Mauricio PochetinoAkitabasamu huku akizidi kuiombea mabaya Chelsea huku yeye ambae timu yake iliwafumua Bournemouth siku ya jumamosi kwa goli 3-0 akizidi kujipanga kushinda kila.mechi.

Ligi hiyo itaendelea usiku wa Leo wakati Arsenal ya Mzee Wenger itakaposafiri mpaka riverside stadium kupapatuana na wenyeji wao Middlesbrough.

Msimamo wa Timu 4 za juu ni huu hapa;

1.Chelsea ....      point 75
2. Tottenham.... Point 71
3. Liverpool...     .Point 66
4.Man city.......      Point 64.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top