SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: YANGA: WAARABU WANAFIA HAPAHAPA TAIFA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kikosi cha Yanga Baada ya kuzungumzwa mengi kuhusu timu ya Yanga kutaka kuukimbia Uwanja wa taifa na kupeleka mechi yake ya kimataifa dh...
Kikosi cha Yanga
Baada ya kuzungumzwa mengi kuhusu timu ya Yanga kutaka kuukimbia Uwanja wa taifa na kupeleka mechi yake ya kimataifa dhidi ya MC Alger ya Algeria kanda ya ziwa mkoani Mwanza, hatimae leo uongozi wa Yanga umekata mzizi wa fitna.

Akizungumza na SDF Sports muda mfupi uliopita, mjumbe wa kamati ya utendaji ya Yanga Salum Mkemi amesema mechi za Yanga za kimataifa zitaendelea kuchezwa hapa hapa Dar es Salaam mpaka watakapoona kuna umuhimu na ulazima wa kuhamishi mechi hizo sehemu nyingine.

"Mechi zetu za kimataifa tutaendelea kuchezea hapa hapa Dar es Salaam na hakuna kiongozi aliwahi kuzungumza kwamba tutapeleka timu CCM Kirumba mkoani Mwanza. Hata kama yupo kiongozi alisema hivyo, taarifa hizo hazikuwa rasmi." alisema

Pia Mkemi alizungumzia maendeleo ya timu katika maandalizi ya mchezo wa ligi dhidi ya Azam FC Jumamosi hii. "Timu inaendelea na mazoezi na majeruhi wengi wamepona amebaki Ngoma bado anaendelea na matibau".

Yanga ina mchezo mgumu wa ligi Jumamosi tarehe moja mwezi ujao dhidi ya Azam FC. Baada ya hapo wataendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wa kimataifa wa kombe la shirikisho barani Afrika, mchezo utakaochezwa mwezi wa 4 kati ya tarehe 7-9.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top