SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA NA MADINI ZAVUNJA REKODI YA MAPATO ARUSHA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho  kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya machàlii wa Arusha,Madini Sc imeingiza kiasi cha ...
Mechi ya robo fainali ya kombe la shirikisho  kati ya Wekundu wa Msimbazi Simba dhidi ya machàlii wa Arusha,Madini Sc imeingiza kiasi cha Shilingi Milioni  81na kuvunja rekodi ya mapato kwani mashindano hayo hayajawah kuingiza kiasi hicho katika uwanja huo katika miaka ya hivi karibuni.

Mechi hiyo ambayo iliisha kwa wekundu wa msimbazi kuibuka na ushindi wa goli 1-0 likifungwa na mshambuliaji hatari raia wa Burundi Laudit Mavugo , liliwafanya Simba kukata tiketi ya kuingia nusu fainali.

Mgawanyo wa mapato hayo ulikuwa kama.ifuatavyo:
Simba na Madini kila mmoja alipata tsh mil 17,TFF iliingiza Tsh mil 12 na chama.cha soka mkoa wa Arusha chenyewe kiliambulia kiasi cha Tsh mil 3.

Mapato hayo yameonyesha namna mashabiki wa soka wa Arusha na maeneo ya karibu, walivyokosa ladha ya mechi kubwa kwa muda mrefu hivyo hiyo ndio ilikuwa fursa yao ya pekee kuwashuhudia wekundu hao wa msimbazi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Ukisikia tumia fursa ndo uku,viongozi kazeni buti umoja upendo mshikamano ndo silaha kuelekea kua machampions wa ligi kuu ya bara.

    ReplyDelete

 
Top