Mabingwa ligi kuu Vodacom Tanzania Bara na wawakilishi pekee katika michuano ya
kimataifa Young Africa itamenyana na Mc
Alger ya Algeria katika mchujo wa kuwania hatua ya makundi ya kombe la
shirikisho Afrika.
Hii ni baada ya droo iliyofanyika mchana huu mjini Cairo
Misri makao makuu ya shirikisho la soka Afrika (Caf).
Yanga imeangukia kombe la shirikisho baada ya
kuondoshwa katika michuano ya ligi ya
mabingwa baada ya kupata sare ya bila kufungana na wenyeji Zanaco katika mchezo
wa marejeano uliofanyika lusaka Zambia katika uwanja wa mashujaa.
mchezo wa awali Yanga akiwa mwenyeji alilazimishwa
sare ya bao 1-1 na matokeo hayo Yanga ilijikuta ikiondoshwa katika michuano ya
ligi mabingwa kwa mabao ya ugenini.
Yanga itaanza kucheza mchezo wake wa kwanza wa kombe
la shirikisho Jijini Dar Es Salaam kati
ya April 7 hadi 9 na mchezo wa marejeano utapigwa April 14 hadi 19 nchini
Algeria.
Post a Comment