Mabingwa watetezi wa kombe la ligi kuu ya soka
Tanzania Bara, Yanga,
kesho wanatarajia kufahamu ni timu gani
itakayopambana nayo katika mechi mbili za mtoano ili kupata nafasi ya kuingia
katika hatua ya makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Africa, wakati ratiba ya
mechi hizo itakapopangwa hapo kesho katika Makao Makuu ya CAF yaliyoko Cairo
nchini Misri.
Mzunguko huo wa timu 16 itakutanisha timu
zilizoondolewa kwenye hatua ya pili ya Ligi ya Mabingwa Barani Africa na timu
zilizofuzu katika hatua hiyo ya kwanza kwa mwaka 2017 kutoka kombe la
shirikisho.
Yanga inaenda kwenye Kombe la Shirikisho baada ya
kutolewa kwa sheria ya goli la ugenini na Zanaco ya Zambia, baada ya suluhu ya bila kufungana
katika mechi iliyofanyika juzi nchini Zambia.
Timu zingine zilizoangukia kwenye Kombe la
Shirikisho ni RC Kadiogo (Burkina Faso), AC Leopards (Congo), AS Tanda (Cote
d’Ivoire), TP Mazembe (DR Congo), Mounana (Gabon), Gambia Ports Authority
(Gambia), Horoya (Guinea), CNaPS (Madagascar), AS Port Louis (Mauritius), FUS
Rabat (Morocco), Barrack Young Controllers (Liberia), Rivers United, Rangers
(Nigeria), Bidvest (South Africa),
Wakati timu zilizofuzu kutoka katika hatua ya kwanza
ya kombe la shirikisho ni MC Alger, JS Kabylie (Algeria), Recreativo do Libolo
(Angola), ASEC Mimosas (Cote d’Ivoire), El Masry, Smouha (Egypt), MAS Fes,
Ittihad Tangier (Morocco), Rayon Sports (Rwanda), Hilal El Obeid (Sudan),
Mbabane Swallows (Swaziland), Platinum Stars, Supersport (South Africa), Club
Africain, CS Sfaxien (Tunisia), Zesco United (Zambia).
Mechi za kwanza zitapigwa kati ya tarehe 7-9 April
na mechi za marudiano zitakuwa kati ya tarehe 14-16 April.
Kila la kheri wawakilishi pekee wa Tanzania katika
michezo ya vilabu barani Africa


Post a Comment