SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NILIZUIA HISIA ZANGU ASEMA DEFOE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa Timu ya Sunderland inayopigania kutokushuka daraja Jermain Defoe amesema alijitahidi kuzuia hisia zake kabla na baada ya k...
Mshambuliaji wa Timu ya Sunderland inayopigania kutokushuka daraja Jermain Defoe amesema alijitahidi kuzuia hisia zake kabla na baada ya kufunga Goli la kwanza kwa Uingereza kwa sababu ya uwepo wa mtoto anaesumbuliwa na ugonjwa wa saratani Bradley Lowrey

Bradley ni shabiki mkubwa wa Sunderland na shabiki mkubwa wa Defoe, aliingia uwanjani akishikwa mkono na Defoe wakati Uingereza ilipopambana na Lithuania.
Kikawaida nahodha ndio husimama mbele kwa ajili ya kuwaongoza wenzie lakini Golikipa Joe hart ambae ndio alikuwa nahodha wa mechi hiyo alimpisha mbele Defoe na Bradley ili wawaongoze wachezaji.

Mtoto Bradley anasumbuliwa na ugonjwa wa saratani na ilihisiwa maisha yake yangefika ukingoni toka mwanzoni mwa mwezi February lakini kwa kudra za mungu hadi Leo bado anaishi.
Katika mechi hiyo Uingereza ilishinda kwa magoli mawili kwa sifur huku goli lingine likifungwa na Jamie Vardy na kuifanya Timu hiyo kuwa kinara wa kundi F katika mbio za kuelekea Urusi mwaka 2018.

Ikumbukwe Defoe (34) ameitwa kwa Mara ya kwanza toka alivyocheza kwa Mara ya mwisho miaka minne ilopita.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top