SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: ITAKUWA MECHI NGUMU KWANGU ASEMA MAVUGO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi na Simba Laudit Mavugo amezungungumzia mchezo wakesho wa Taifa stars dhidi ya Burundi utakao chez...
Mshambuliaji wa timu ya taifa ya Burundi na Simba Laudit Mavugo amezungungumzia mchezo wakesho wa Taifa stars dhidi ya Burundi utakao chezwa uwanja wa Taifa Dar es salam

Akiongea jioni hii kabla yamazoezi ya mwisho na timu yake alisema, mechi itakua ngumu kwangu kwasababu nacheza na wachezaji tunao juana na wengine nacheza nao timu moja. 

"Mechi itakuangumu sana hasa kwangu kwasababu nacheza na wachezaji ambao tunajuana vizuri na wengi wao tunacheza Timu moja lakini ngoja tuone itakavyo kua kesho naamini kuna Warundi wapo hapa waje waone timu yao."alisema

Lakini pia Mavugo alizungumzia ubora wa Taifa Stars kwamba nitimu nzuri ina mchanganyiko wa vijana wengi wanao ujua mpira. 

Niliangalia mechi yao dhidi ya Botswana kipindi cha kwanza walicheza vizuri na walistahili kushinda, nakesho wakijituma wanaweza wakafanya vizuri".alisema

Taifa Stars kesho inacheza mchezo mwingine ambao upo kwenye kalenda ya FIFA baada ya juzi jumamosi kuitandika Botswana goli mbili kwa bila.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top