SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: TUMEKUJA KUWASHANGAZA WATANZANIA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Burundi  Niyungeko Aloin Olivier amesema wamekuja Kuishangaza Tanzania japokuwa anajua mechi itakuwa ngumu...

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Burundi  Niyungeko Aloin Olivier amesema wamekuja Kuishangaza Tanzania japokuwa anajua mechi itakuwa ngumu sana,Nimesikia wamecheza na  Botswana,wana timu nzuri na wana wachezaji wa kulipwa,hasa mchezaji wao Mbwana samata anaecheza ulaya,nataka nione namna wachezaji wangu watakavyokabiliana nae,aliongeza kocha huyo.

Mechi hiyo inayotazamiwa kuchezwa kesho ikiwa ni katika kalenda za FiFa itashuhudia Burundi wakiivaa Tanzania siku Takriban mbili baada ya Tanzania kuifunga  Botswana kwa magoli mawili kwa bila.

Kocha huyo aliongeza pia,Tumetoka.kucheza na Djibouti na kuwafunga goli 7 katika mechi ya kwanza na ya pili goli moja,tumejiandaa Vizuri kuwakabili Tanzania.

Nae Nahodha wa Timu hiyo Harelimana Rachid Leon amesema wamekuja kuifunga Tanzania japokuwa watanzania wengi wanaonekana kuidharau timu yao kwa kuwa wana wachezaji wenye maumbo madogo,Ni kweli wachezaji wengi wa Burundi wana maumbo madogo lakini wana akili nyingi ya mpira hivyo Tanzania isitegemee kupata urahisi katika mechi hiyo.

Nae mkurugenzi wa benchi La Ufundi LA Burundi na mkuu wa msafara,amesema.wamekuja kucheza na Tanzania kwa kuwa wana mahusiano mazuri na sisi,na wameleta vijana wengi ambao wanawaandaa kwa ajili ya michezo ya Chan na Afcon.
Burundi pia itaongozwa na mshambuliaji hatari wa Wekundu wa Msimbazi Laudit Mavugo ambae ameapa lazima awafunge Tanzania.

Kiingilio cha Chini katika mechi hiyo kitakuwa ni Shilingi elfu 3.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top