![]() |
Mwesigwa na Anjela Mzirai |
Kaimu mkurugenzi wa mfuko huko Anjela Mzirai amesema bima hiyo itakuwa ni faida kubwa kwa wachezaji hao kwakuwa itawasaidia kupata huduma ya afya popote nchini hata kama wasipokuwa kambini.
Mzirai amewataka wachezaji hao wa Serengeti Boys kuwa mabalozi wa kuhamasisha vijana wengine kujiunga kwenye mfuko huo, ambao una vituo zaidi ya 6000 huku mfuko huo ukiwa umesambaa kwa zaidi ya asilimia 90 nchini.
"Kwa niaba ya NHIF napenda kuushukuru uongozi wa Shirikisho la mpira TFF chini ya uongozi wa Rais Jamal Malinzi kwa kufanikisha suala hili" alisema Mzirai.
Mzirai alisema kuwa "NHIF itaendelea kushirkiana na TFF katika masuala mbalimbali kama ilivyo katika ligi kuu ya Vodacom".
![]() |
Wachezaji wa Serengeti Boys katika hafla ya kukabidhiwa kadi za NHIF |
Kwa upande wake katibu mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa amesema wataendelea kuhamasisha vijana wengi zaidi kujiunga na mfuko huo kutokana na umuhimu wake.
Post a Comment