Kocha wa Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Salum Mayanga, amesema mechi ya kesho ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya Botswana, itampa mwanga kuelekea michuano ya kufuzu mataifa ya Afrika mwezi Juni.
Stars itashuka dimbani kesho saa kumi jioni kumenyana na Botswana katika mchezo huo uliopo kwenye kalenda ya FIFA.
"Ni mchezo wangu wa kwanza katika mwaka huu na mechi hii itanipa mwanga kuangalia vizuri kikosi kabla ya kuanza kwa mechi za mwezi Juni," alisema Mayanga.
Naye nahodha wa timu hiyo Mbwana Samatta alisema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo, ili kuleta heshima kwa Taifa na kusaidia kupanda kwenye viwago vya FIFA.
"Tumejipanga vizuri kwa mchezo tunaimani tutashinda ili kuleta furaha na heshima kwa Watanzania, Mwalimu ameita wachezaji ambao ameona wanafaa kikubwa ni kuwa tunahitaji sapoti kutoka kwa Watanzania" alisema Samata.
Kiingilio cha chini kwenye mchezo kitakuwa shilingi 3000 ili kuwafanya watanzania wajitokeze kwa wingi kuisapoti timu yao.
About Author

Advertisement

Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Mimi ni Mzalendo.Nitakuwepo uwanjani kutoa support kwa Taifa Stars.
ReplyDelete