SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MWAMUZI SIMBA NA MBEYA CITY APEWA ONYO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kamati ya masaa 72 ya TFF imempa onyo kali mwamuzi Jakob Adongo aliyechezesha mechi ya Simba na Mbeya city kwakosa la kushindwa kutafsiri ...
Kamati ya masaa 72 ya TFF imempa onyo kali mwamuzi Jakob Adongo aliyechezesha mechi ya Simba na Mbeya city kwakosa la kushindwa kutafsiri sheria 17 za mpira wa miguu Machi 4 kwenye uwanja wa Taifa.

Vile vile Kamati hiyo imepiga faini shilingi 500,00 timu ya Mbeya City baada ya kuingia kwenye mlango usio rasmi na kukikuka kanuni za ligi.

Akiongea na waandishi wa habari leo msemaji wa TFF Alfred Lucas alisema Kamati hiyo imepitia makosa mbalimbali yalijitokeza na kutoa adhabu ambapo Adongo amepewa onyo kali huku Mbeya City wakilimwa faini.

"Mwamuzi Adongo amepewa onyo kali kwakushindwa kutafsiri vizuri sheria 17 za soka lakini City wamepigwa faini ya shilingi laki tano kuvuja kanuni za ligi," alisema Lucas.

Lucas alisema pia timu ya Majimaji imepigwa faini ya shilingi 300,000 baada ya kushindwa kupeleka daktari kwenye mkutano kabla ya mchezo dhidi ya Kagera Sugar.

Lakini pia kamati hiyo imefuta kadi ya njano aliyopewa Jafari Salum wa Mtibwa Sugar kwenye mechi dhidi ya African Lyon sababu ilitolewa na mwamuzi kimakosa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top