SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: NAPE AMFUNIKA MGENI RASMI DR. MWAKYEMBE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nape Moses Nnauye akiwasalimia mashabiki katika uwanja wa taifa hapo jana  Aliyekuwa waziri wa habari utamaduni na michezo Nape Moses Nn...
Nape Moses Nnauye akiwasalimia mashabiki katika uwanja wa taifa hapo jana
 Aliyekuwa waziri wa habari utamaduni na michezo Nape Moses Nnauye leo alipokewa kwa shangwe la aina yake katika uwanja wa taifa jijini Dar es Salaam mara baada ya kusimama katika kiti alichokuwa amekaa katika eneo la VIP A, wakati wa mapumziko katika mchezo baina ya timu ya taifa ya Tanzania maarufu kama Taifa Stars dhidi ya Botswana.

Mapema wiki hii rais Dr. John Magufuli alifanya mabadiliko katika baraza lake la mawaziri na kumtoa mbunge wa jimbo la Mtama Nape Nnauye katika nafasi ya waziri wa habari utamaduni na michezo na nafasi yake kuchukuliwa na Dr. Harrison Mwakyembe.

Dr. Mwakyembe ndiye alikuwa mgeni rasmi katika mchezo wa leo ambapo Taifa Stars wameibugiza Botswana magoli mawili kwa bila, huku magoli yote yakifungwa na mshambulizi wa KRC Genk ya ligi kuu nchini Ubelgiji, Mbwana Ally Samatta. Dr. Mwakyembe aliingia uwanjani kabla ya mchezo huo kuanza na kusalimiana na timu zote mbili pamoja na marefarii wa mchezo huo, huku akipigiwa makofi na mashabiki waliojitokeza katika mchezo huo.

Katika kile kilichotafsiriwa na wengi kuwa ni kukubalika na wadau wa sekta ya habari na michezo wakati akiitumikia wizara husika kama waziri, aliyekuwa waziri wa wizara hiyo Nape Nnauye alishangiliwa sana alipojitokeza katika jukwaa la VIP A huku mashabiki wote uwanjani hapo wakiimba "NAPE NAPE NAPE" pindi tu walipomuona. Hali iliyomlazimu Nape kuwasogelea mashabiki wa pande zote za uwanja wa taifa na kuwasalimu kwa kupunga mkono huku baadhi waliokuwa karibu nae wakipiga nae picha.




About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top