SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MSUVA ACHEKELEA SANA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Msuva akishangilia bao la kwanza la Samatta pamoja na Samatta   Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuibuka na ushindi wa mag...
Msuva akishangilia bao la kwanza la
Samatta pamoja na Samatta  
Baada ya timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars kuibuka na ushindi wa magoli mawili kwa bila dhidi ya Botswana, winga wa timu hiyo Simon Msuva amefurahia sana magoli mawili ya Mbwana Samatta aliyofunga.

Akiongea baada ya mechi hiyo kuisha Msuva alisema amefurahi sana kuona Samata amefunga magoli mawili na muhimu kwa timu haswa kwa kuzingatia hajaifungia Taifa Stars goli kwa muda mrefu.

"Nimefurahi kuona Samatta amefunga magoli muhimu kwenye mechi hii ambayo ipo kwenye kalenda ya FIFA ukizingatia kuwa ana muda mrefu kidogo hajaifungia Stars goli. Lakini pia Timu nzima tumecheza kwa ushirikiano mzuri sana leo kila mmoja alikuwa anajituma, inaleta faraja na ukizingatia kikosi hiki ni kipya na kina vijana wengi pamoja na kocha mpya"

Kwa upande mwingine kocha wa timu hiyo Salum Mayanga akizungumzia mchezo huo alisema vijana wake wamejitahidi na wamecheza vizuri wakapata goli la mapema. Japo wapinzani wake walitawala eneo la kiungo hali iliyomlazimu kubadilisha mfumo na kumuingiza winga wake mmoja acheze katikati ya uwanja ili kujaribu kuwadhibiti Wabotswana.

Mayanga alinukuliwa akisema kuwa "vijana wamejitahidi wamecheza vizuri na kufanikiwa kupata goli la mapema lakini wapinzani wetu walitukamata sehemu ya kiungo cha kati hali iliyonilazimu kubadilisha mfumo na kumuingiza winga mmoja katikati, Naomba nipewe muda niendelee kuirekebisha hii timu haswa eneo la kiungo." alisema.

Stars itacheza tena mchezo mwingine wa kirafiki siku ya jumanne dhidi ya Burundi katika uwanja huo huo wa Taifa majira ya saa kumi za jioni.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top