SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SAMATTA AIBEBA STARS ATUPIA MBILI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Kapteni wa Taifa Stars akishangilia na wenzake moja ya magoli yake dhidi ya  Botswana leo Timu ya soka ya Taifa yaTanzania Taifa Stars i...
Kapteni wa Taifa Stars akishangilia na
wenzake moja ya magoli yake dhidi ya
 Botswana leo
Timu ya soka ya Taifa yaTanzania Taifa Stars imeitandika timu ya Taifa ya Botswana magoli  2-0 katika mchezo Wa Kirafiki Wa kimataifa uliochezwa uwanja wa taifa jijini Das es Salaam hii leo.

Iliwachukuwa Stars dakika mbili tu kuandika bao la kwanza, kupitia kwa mshambulizi wake hatari anayecheza soka ya kulipwa barani ulaya nchini Ubelgiji katika klabu ya KRC Genk Mbwana Ally Samatta, akimalizia pasi murua kutoka kwa mchezaji Shiza Ramadhan Kichuya.

Gili hilo liliwazindua Botswana, wakaja juu kutaka kusawazisha hali hiyo iliifanya Stars kuonekana kuzidiwa katika sehemu ya katikati ya uwanja, lakini  safu yake ya ulinzi iliyokuwa chini ya Abdi Banda na Erasto Nyoni ilikuwa imara na kuwadhibiti vilivyo Wabotswana.

Katika dakika ya 19 mchezaji wa Botswana Lesenya Ramoraka aliumia na kutoka nje na nafasi yake kuchukuliwa na Thero Setsile. Mabadiliko hayo yalionekana kuisaidia sana Botswana kwani Thero alikuwa mzuri kupandisha mashambulizi.

 Katika dakika ya 23 almanusura Banda aipatie Stars goli la pili kwa kichwa, akiunganisha kona iliyochongwa na Shiza Kichuya

 Lebonga Ditsele wa Botswana dakika ya 33 alishindwa kuisawazishia timu yake goli baada kugongesha mpira kwenye mwamba wa kushoto kwa golikipa Aishi Manula baada ya kuunganisha krosi safi ya Thero Setsile, hadi kipindi cha kwanza kinamalizika Stars 1-0 Botswana

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huko Botswana wakionekana hatari zaidi katika dakika za mwanzo, hali iliyomlazimu mwalimu wa Stars Salum Mayanga kufanya mabadiliko katika dakika ya 53 kwa kumtoa Frank Domayo na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yasin.

Kuingia kwa Mzamiru kuliiamsha Stars haswa eneo la katika na kuanza kulisakama lango la Botswana kama nyuki.

Dakika 3 tu tangu aingie Mzamiru Yasin alimpelekea Simon Msuva pasi safi iliyomkuta akitazamana na golikipa wa Botswana Kabelo Dambe, aliyepangua shuti la Msuva na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda kwa upande wa Stars.

Katika dakika 57 Simon Msuva tena alikosa goli akiwa yeye na lango la Botswana kufutia krosi ndogo safi kutoka kwa Mbwana Ally Samatta alitokea katikati ya uwanja na mpira akiwahadaa wachezaji wa Botswana mmoja baada ya mwingine.

Golikipa wa Botswana Dambe alifanya kazi ya ziada katika dakika ya 77 na kupangua shuti la karibu la Mbwana Samatta ndani ya eneo la hatari kufuatia kazi nzuri ya mchezaji Farid Mussa anayekipiga katika klabu ya Tenerife ya nchini Hispania, aliyeingia katika dakika ya 59 kuchukua nafasi ya Shiza Ramadhan Kichuya.

Mwamuzi Elly Sasii alimzawadia Thero Setsile kadi ya njano baada ya kumfanyia madhambi Samatta, nje kidogo ya eneo la hatari la Botswana

Alikuwa ni Mbwana Ally Samatta tena aliyeipatia Stars goli la pili,kwa mkwaju wa adhabu ndogo nje kidogo ya box na kuiandikia Stars bao la 2 lililowafanya Botswana kutoka kapa katika uwanja wa Taifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top