Wahenga walinena wakati ukuta usishindane nao na katu haumsubiri mwanadamu. Yawezekana Tff waliutumia msemo huu kufanya maamuzi ya haraka kwa wakati sahihi lakini ikawa tofauti kwa shirikisho la soka la Zambia(Faz).
Wakati ikifahamika kuwa tarehe 25 mwezi huu ni mechi za kimataifa za kirafiki kwa mujibu kalenda ya Fifa, Tff walifanya mawasiliano na shirikisho la soka la Zambia ili timu ya taifa ya nchi hiyo Chipolopolo wawe waalikwa wa Taifa Stars katika tarehe hiyo, mchezo ambao ungevurumishwa katika dimba la Taifa Jijini Dar Es Salaam. Lakini Zambia walikaa kimya kwa siku nyingi na hivyo Tff wakaamua kuchukua tahadhari kwa kusaka mechi nyingine na kutuma maombi shirikisho la soka la Botswana(Bfa) ambao yalikubaliwa na Tff kuitangaza rasmi Botswana kuwa mwalikwa wetu machi 25.
Katika hali ya kushangaza juzi Zambia wamerudisha majibu kwa Tff kuwa wako tayari kukipiga na Stars tarehe 25 machi. Na kuonyesha kuwa wanamaanisha kile walichowajibu juzi TFF, jana wametaja kikosi chao rasmi cha wachezaji 25 wanaojiandaa kuja kukipiga na Taifa Stars.
Kutegua kitendawili hiki mtandao wetu ulimtafuta Afisa wa Tff ambae hakupenda kutajwa jina lake alisema haya; "ni kweli Zambia wametujibu juzi kuwa wako tayari kucheza na sisi tarehe 25 na jana wametaja kikosi chao rasmi cha kuja kucheza na Taifa Stars. Lakini sisi hatuwezi kucheza nao tena tuliwatumia maombi mapema sana walikaa kimya tukawatafuta Botswana wakatujibu mapema tu kuwa wako tayari na tukakubaliana. Hivyo tarehe 25 tutacheza na Botswana sio Zambia, maandalizi yetu yote ni kwaajili ya mwalikwa wetu Botswana". Alinukuliwa Afisa wa Tff akitegua kitendawili hiki.
Hiki ndio kikosi cha wachezaji 25 kilichotajwa jana na shirikisho la soka Zambia kuja kukipiga na Stars.
Makipa: Jacob Banda, Allan Chibwe, Racha Kola
Mabeki; Taonga Bwambya, Donashano Malama, Fackson Kapumbu, Ziyo Tembo, Isaac Samutomba, Billy Mutale, Adrian Chama.
Viungo; Kondwani Mtonge, Meshack Chaila, John Ching'andu, Cletus Chama, Fwayo Tembo, Kelvin Mubanga, Augustine Mulenga.
Washambuliaji; Justine Banda, Mwila Phiri, Mukabanga Siambombe, Jackson Mwama, Chitiya Mususu, Ronald Kampambe.
CHIPOLOPOLO WAJICHANGANYA, WANAJIANDAA KUJA TAIFA
Title: CHIPOLOPOLO WAJICHANGANYA, WANAJIANDAA KUJA TAIFA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Wahenga walinena wakati ukuta usishindane nao na katu haumsubiri mwanadamu. Yawezekana Tff waliutumia msemo huu kufanya maamuzi ya haraka ...
Zambia dharau imewaponza.
ReplyDeleteWazambia wana dharau sana. Eko kwa TFF
ReplyDelete