SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SAMATTA AWAMWAGIA SIFA WACHEZAJI WA KIBONGO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samata amesema kwa sasa kuna wachezaji wengi wa Kitanzania wana uwezo w...

Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' Mbwana Samata amesema kwa sasa kuna wachezaji wengi wa Kitanzania wana uwezo wa kucheza soka barani Ulaya.

Samata alisema hayo muda mfupi kabla ya kuanza kwa mazoezi ya timu ya Taifa yaliyofanyika katika uwanja wa Taifa Dar es Salaam kujiwinda na michezo ya kirafiki dhidi ya Botwasana na Burundi.

Samata ambaye aliwasili usiku wa kuamkia leo alisema kwa sasa kuna wachezaji wengi wenye uwezo wa kucheza Ulaya kilichobaki ni muda tu haujafika kwao.

Samata alisema: "siwezi kutaja mchezaji mmoja mmoja ila ni wengi ambao wanaweza kucheza soka la kulipwa ila muda wao haujafika".

Samata anatajiwa ambaye anacheza soka la kulipwa Ulaya katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji anatarajiwa kuingoza Stars katika mchezo wa kwanza dhidi ya Botswana Jumamosi katika uwanja wa Taifa.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top