Robo Fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports
Federation Cup 2016/2017), kati ya Azam FC na Ndanda FC itafanyika
Aprili 5, 2017 saa 1.00 usiku kwenye Uwanja wa Azam ulioko Chamazi, nje
kidogo ya jiji la Dar es Salaam, imefahamika.
Kadhalika, Robo Fainali ya nne ya mwisho ya Kombe la Shirikisho la
Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Young Africans na
Tanzania Prisons FC itafanyika Aprili 22, 2017 saa 10.00 jioni kwenye
Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Washindi wa kila mchezo watasonga mbele kwenda Raundi ya Nane ambayo
ni Nusu Fainali. Tayari klabu za Mbao na Simba zilitangulia hatua hiyo
ya Nusu Fainali.
Mbao FC ya Mwanza nayo imetangulia hatua ya Nusu Fainali baada ya
kuilaza Kagera Sugar mabao 2-1 katika mchezo wa Robo Fainali ya kwanza
uliofanyika Uwanja wa Kaitaba mkoani Kagera Machi 18, mwaka huu.
Kwa upande wake, Klabu ya Simba ya Dar es Salaam imepita baada ya
kuishinda Madini FC ya Arusha kwa bao 1-0 katika mchezo wa Robo Fainali
ya pili uliofanyika Machi 19, 2017 kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid
jijini Arusha.
AZAM NA NDANDA KUPIGWA APRIL 5
Title: AZAM NA NDANDA KUPIGWA APRIL 5
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Robo Fainali ya tatu ya Kombe la Shirikisho la Azam (Azam Sports Federation Cup 2016/2017), kati ya Azam FC na Ndanda FC itafanyika Apri...
Post a Comment