SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: MERSEYSIDE DERBY UNAIJUA UNAISKIA..?
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ligi mbalimbali Duniani zinarejea tena kuanzia kesho baada ya mapumziko ya kupisha mechi mbalimbali za kimataifa za kirafiki zilizo ka...


Ligi mbalimbali Duniani zinarejea tena kuanzia kesho baada ya mapumziko ya kupisha mechi mbalimbali za kimataifa za kirafiki zilizo katika kalenda ya FIFA pamoja na zile za kufuzu kwa kombe la Dunia litakalofanyika mwakani nchini Urusi.

Wakati hapa nyumbani mechi inayosubiriwa kwa kubwa ni ile itakayowakutanisha miamba miwili ya Yanga na Azam,huko uingereza kuna mechi inayosubiriwa sana ikiwakutanisha mahasimu wawili kutoka jiji la Liverpool ambapo Majogoo wa jiji hilo watakapowakaribisha Kaka zao wa Everton.

Friendly Derby.. Ndivyo inavyofahamika zaidi kwa maana ndio derby pekee duniani inayowakutanisha wanandugu,wanafamilia,majirani kwenye vita ya dakika 90 kisha baada ya hapo maisha yanaendelea kama kawaida,ni jambo la kawaida kukuta familia moja imegawanyika.Mara mbili,blue au nyekundu,lakini wakifika uwanjani wanageuka maadui.
Hata wachezaji kadhaa ambao wamezichezea timu hizi wamekuwa na mapenzi ya tofauti na timu walizochezea,mfano ni Jamie caragher aliyechezea zaidi ya mechi 600 na Liverpool huku akiwa ni mshabiki wa kutupwa wa Everton.

Taarifa Muhimu kuhusu mechi hii.

Timu hizi zinakutana Mara ya 277 na Liverpool ikishinda mechi 90 huku Everton ikishinda mechi 66 tu huku wakienda sare mechi 77.

Vurugu ndani ya uwanja.
Pamoja na kuwa mechi hii inafahamika kama ya kirafiki nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja imekuwa na patashika kubwa sana kiasi imeweka historia ya derby ilozalisha kadi nyekundu nyingi sana ambazo ni 21 huku Steven Gerard nahodha wa zamani wa Liverpool na Phile Nevile ambae nae pia ni nahodha wa zamani wa Everton wakiongoza kwa kupewa kadi nyekundu 2 katika mechi tofauti.

Ian Rush anaongoza kwa kufunga magoli mengi katika mechi hizi ambapo amefunga magoli 25.

Ushindi mkubwa kwa timu hizi ni ule wa mwaka 1935 ambapo Liverpool alishinda kwa goli 6 kwa sifuri.

Ikumbukwe kuwa Everton walikuwa wakitumia uwanja wa anfield kabla ya kuzinguana na wamiliki wa uwanja kutokana na kuwapandishia kodi ,ndipo walipojenga uwanja wao wa Goodison Park ambao unapakana karibu kabisa na Anfield,umbali kutoka anfield kwenda Goodison Park ni chini ya maili moja.

Pia Kama ulikuwa hujui..Jiji la Liverpool ndio jiji lenye mafanikio makubwa ya soka nchini uingereza kwani timu hizi mbili zimechukua jumla ya makombe 27 ya ligi kuu,

Mechi hiyo ya kesho inatarajia kuanza mida ya 9 na nusu kwa Saa za Africa Mashariki,je nani ataibuka mbabe...ni jambo la kusubiri na kuona.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. May the best team win tomorrow......YNWA YNWA...WE ARE LIVERPOOL

    ReplyDelete

 
Top