SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: SIMBA YAWAPIGISHA KWATA WANAJESHI WA RUVU
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Timu ya soka ya Simba sc leo hii imeendleza ubabe wake baada ya kuipiga timu ya Ruvu Shooting kwa magoli 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya ...
Timu ya soka ya Simba sc leo hii imeendleza ubabe wake baada ya kuipiga timu ya Ruvu Shooting kwa magoli 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya vodacom uliochezwa leo hii katika uwanja wa Uhuru.

Ruvu shooting ilikuwa ya kwanza kupata goli dakika ya 8 kupitia mshambuliaji wake Abdulrahman Mussa aliyepiga shuti kali nje ya 18 shuti liliomzidi golikipa wa Simba,Vicent Angaban. Dakika tatu baadae Simba ilisawazisha kupitia Ibrahim Ajibu aliyeunganisha vyema krosi ya Mohamed Hussein'Zmbwe'. Katika dk ya 19 Laudit Maugo alipoteza nafasi ya wazi akiwa amebaki na kipa wa Jkt Ruvu Abdallah Rashid. Katika dk ya 23 Simba ilipoteza tena kupitia Mavugo aliyeshindwa kuunganisha vyema pasi ya Ibrahim Ajibu na katika dakika ya 31 Said Ndemla wa Simba alipiga shuti lakini kipa wa Ruvu shooting Abdallah Abdallah aliokoa shuti lile kwa kulipangua. Mavugo alipoteza nafasi nyingine ya wazi kwa kupaisha tena mpira. mpaka halftime matokeo yalikuwa 1-1. Katika kipindi cha kwanza mwamuzi Ngole Mwangole alitoa kadi mbili za njano moja akimpa mchezaji wa Simba Ibrahim Hajibu na upande wa Ruvu shooting alimpa kadi Frank Msese

Katika kipindi cha pili,Simba ilianza kwa kucheza kwa kasi sana na ikaweza kufanikiwa kupata goli la pili la mchezo katika dakika ya 48 kupitia mshambuliaji wake Laudit mavugo aliyeunganisha vyema pasi ya Ibrahim Hajibu. Katika dakika ya 62,Mwamuzi Ngole Mwangole alitoa kadi nyekundu na kumpa Jabir Aziz wa Ruvu shooting kutokana na kumchezea rafu Ibrahim Ajibu. Katika dakika ya 64 Simba ilifanya mabadiliko ilimtoa Mavugo na nafasi yake ikachukuliwa na fredrick Blagnon. Katika dakika ya 73 Ibrahim Hajibu alipiga shuti lakini liligonga mwamba. Mpaka mpira unaisha matokeo yalibaki 2-1. Mpaka sasa Simba imecheza mechi 3 na imeshinda mechi 2 nakutoka sare mechi moja.

About Author

Advertisement

Post a Comment

  1. Say Bravo to Simba Sports Club
    Tuendele Kudumisha Mshikamano tulionao sasa Mambo mazuri yanakuja

    ReplyDelete
  2. Game ilikuwa poa,ila tunakosa sana nafasi

    ReplyDelete
  3. Game ilikuwa poa,ila tunakosa sana nafasi

    ReplyDelete
  4. Ni kweli @Ntimizi kocha anatakiwa ashughulikia tatizo la umaliziaji kwani tunatengeneza nafasi nyingi lakini tunakosa magoli nadhani kocha amelione hilo.

    ReplyDelete
  5. Kabisa,hlf ajib aongeze nidhamu kidogo maana karibu kila game anapata yellow card

    ReplyDelete

 
Top