SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: USHINDI WA MBAO WAIONGEZEA 'CONFIDANCE' YANGA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Ushindi wa bao moja uliopata timu ya Yanga dhidi ya Mbao FC umerejesha hali ya kujiamini katika kikosi cha mabingwa hao wa zamani wa ligi ...
Ushindi wa bao moja uliopata timu ya Yanga dhidi ya Mbao FC umerejesha hali ya kujiamini katika kikosi cha mabingwa hao wa zamani wa ligi kuu.

Kabla ya mchezo huo Yanga ilikuwa imekubali vipigo katika michezo minne kitu ambacho kilishusha morali ya wachezaji.

Kaimu kocha mkuu wa klabu hiyo, Noel Mwandila amesema ushindi huo ulikuwa muhimu na umerejesha hali ya kujiamini na itawasaidia kufanya vizuri katika michezo miwili ya ligi iliyosalia.

Mwandila ameongeza kuwa mchezo ulikuwa mgumu na timu zote zilicheza vizuri lakini wachezaji wake walifuata maelekezo yake vizuri.

"Ushindi wa leo ni muhimu kwetu na umerejesha hali ya kujiamini kwa wachezaji na tuna imani tutafanya vizuri katika mechi zetu zilizobaki," alisema Mwandila.

Keshokutwa Ijumaa Yanga itashuka tena dimbani kucheza na Ruvu Shooting kabla ya kumaliza ligi na Azam FC Jumatatu ijayo.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top