Klabu ya Simba imepitisha mabadiliko ya katiba kutoka umiliki wa wanachama kwenda kwenye hisa kwa asilimia 98 katika mkutano wa dharura uliofanyika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Nyerere Convention Center leo hii.
Mkutano huo ulihudhuriwa na Waziri Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe ambaye alikuwa mgeni rasmi.
Hii inaama kuwa mwekezaji atapaswa kumiliki hisa asilimia 49 na wanachama watabaki na asimilia 51.
Mfanyabiashara Mohammed Dewji 'MO' alishinda zabuni za kuwekeza ndani ya klabu na ilikuwa inasubiriwa mabadiliko ya katiba ambayo yamekamilika leo na mchakato unaendelea.
MO atawekeza hisa asilimia 49 zenye thamani ya shilingi bilioni 20 na kuifanya Simba kuendeshwa kisasa.
SIMBA YAPITISHA MABADILIKO YA KATIBA KWA KISHINDO
Title: SIMBA YAPITISHA MABADILIKO YA KATIBA KWA KISHINDO
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Klabu ya Simba imepitisha mabadiliko ya katiba kutoka umiliki wa wanachama kwenda kwenye hisa kwa asilimia 98 katika mkutano wa dharura ul...
Post a Comment