Serikali imekubali moja kwa moja kwa klabu ya Simba kubadili mfumo wa uendeshwaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda kwenye hisa.
Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Dk. Harrison Mwakyembe katika mkutano mkuu wa dharura wa wanachama uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano Mwalimu Nyerere Convention Center.
Dk. Mwakyembe amesema Serikali haijawahi kukataa mabadiliko kwa klabu yoyote isipokuwa imekuwa ikiagiza kufuatwa utaratibu wa sheria za nchi na katiba ya klabu husika.
Waziri huyo amesema mfumo wa hisa kwa sasa haukwepeki kwakua ni wakibiashara na upo katika soka la kisasa duniani kote na ili timu kufanikiwa haina budi kuingia katika mfumo huo.
"Serikali imeridhia mabadiliko haya ambayo yanaelekea kukamilika kwakua sheria na taratibu za nchi zimefuatwa na kwakua mwekezaji anapaswa kuchukua asilimia 49 na klabu inabaki na 51 hakuna tatizo," alisema Dk. Mwakyembe.
Bilionea Mohammed Dewji ameshinda zabuni hiyo na anategemewa kuweka hisa asilimia 49 zenye thamani ya sh billioni 20 kama utaratibu ukikamilika.
RASMI SERIKALI KIROHO SAFI YABARIKI MABADILIKO SIMBA
Title: RASMI SERIKALI KIROHO SAFI YABARIKI MABADILIKO SIMBA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Serikali imekubali moja kwa moja kwa klabu ya Simba kubadili mfumo wa uendeshwaji kutoka umiliki wa wanachama kwenda kwenye hisa. Kauli ...
Post a Comment