SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KOSCIELNY NJE MIEZI SITA
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Meneja Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa mlinzi Laurent Koscielny atarejea uwanjani mwezi Disemba baada ya kuumia kifundo cha mguu...
Meneja Arsenal, Arsene Wenger amethibitisha kuwa mlinzi Laurent Koscielny atarejea uwanjani mwezi Disemba baada ya kuumia kifundo cha mguu.

Mfaransa huyo atakaa nje ya uwanja kwa miezi sita baada ya kufanyiwa upasuaji wa kifundo cha mguu.

Koscielny aliumia katika mchezo wa nusu fainali ya pili ya Europa dhidi ya Atletico Madrid wiki iliyopita waliopoteza kwa bao Moja.

Beki huyo mwenye miaka 32 atakosa fainali za kombe la dunia pamoja na miezi ya mwanzo ya ligi kuu Uingereza.

"Koscielny atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu anatakiwa kuwafanyiwa upasuaji itamchukua wiki sita nadhani mpaka Disemba ndio atarejea uwanjani," alisema Wenger.

Koscielny, ameichezea Ufaransa mechi 51 na alipanga kustaafu baada ya fainali za kombe la dunia mwezi ujao litakalofanyika nchini Urusi.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top