SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KAPOMBE: BADO SIJAFIKIA KIWANGO CHANGU, MSIMU UJAO MTAFURAHI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mchezaji kiraka wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amewaambia wapenzi na mashabiki wa mabingwa hao kuwa msimu ujao atakuwa bora zaidi baada...
Mchezaji kiraka wa timu ya Simba, Shomari Kapombe amewaambia wapenzi na mashabiki wa mabingwa hao kuwa msimu ujao atakuwa bora zaidi baada ya kuandamwa na majeruhi.

Kapombe alikaa nje ya uwanja kwa muda mrefu kuuguza jeraha la goti ambapo mzunguko wa kwanza wote hakucheza mechi yoyote.

Tangu kurejea uwanjani katika mechi za mwanzoni za mzunguko wa pili Kapombe aliingia moja kwa moja kikosi cha kwanza akionyesha kiwango bora.

Kapombe amesema alikuwa mmoja wa wachezaji wa Simba waliochukua ubingwa mwaka 2011 na amerejea tena msimu huu wakitwaa ubingwa tena kitu ambacho kinamfanya kujiona mwenye bahati.

"Msimu huu haukuwa mzuri sana kwangu, nilipata maumivu yaliyo niweka nje muda mrefu.

"Bado sijarudi kwenye kiwango changu nilichokizoea nawaahidi msimu ujao nitakuwa bora zsidi kuliko hivi," alisema Kapombe.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top