Feisal Salum was kwanza kutoka kushoto mwenye jezi namba 3 |
Katibu mkuu wa klabu hiyo, Sadu Judu amesema ikibainika Singida imemsainisha kiungo huyo wataishitaki ambapo adhabu yake huenda ikawa ni kufungiwa kusajili kwa miaka kadhaa.
Kiongozi huyo amesema Feisal amebakikisha miaka miwili katika mkataba hivyo kikanuni hawezi kusajiliwa na timu nyingine bila kufuatwa utaratibu ukiwemo kuvunjwa mkataba huo.
"Tumesikia taarifa kuwa Singida imemsainisha kiungo wetu Feisal Salum lakini wamefanya jambo ambalo sio zuri kwakua mchezaji bado ana mkataba mrefu wa miaka mitatu.
"Nadhani Singida ilipaswa kutufuata na kukaa chini kuangalia tunafanyaje juu ya usajili wake lakini wakileta ubabe wasitulaumu kwa kitakacho watokea," alisema Judu.
Kipaji cha Feisal kilionekana vizuri katika michuano ya Cecafa Chalenji iliyofanyika nchini Kenya akiwa na timu ya Zanzibar Heroes iliyoingia hadi fainali mwezi Novemba mwaka jana.
Post a Comment