SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: KARIBU MSIMBAZI SPORTS PESA…LAKINI
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Zilianza kama tetesi kwa mashabiki wa soka Tanzania juu ya ujio wa kampuni ya kuchezesha michezo ya kubashiri ya Sport pesa ya Kenya juu y...
Zilianza kama tetesi kwa mashabiki wa soka Tanzania juu ya ujio wa kampuni ya kuchezesha michezo ya kubashiri ya Sport pesa ya Kenya juu ya kuwekeza na kuendesha mchezo maarufu wa kubashiri matokeo ya michezo mbalimbali duniani,lakini tetesi zaidi zikavuma kwamba kampuni hiyo ambayo pia ndio mdhamini wa klabu ya ligi kuu ya uingereza ya Hull City na huku pia ikiwa imeingia kandarasi ya kuidhamini klabu nyingine ya uingereza ya Everton imeingia kandarasi ya udhamini kwa vilabu vya simba na Yanga.

Tetesi hizo zilianza kushika chati kwa takribani juma zima mpaka hapo jana ijumaa zilipozaa ukweli na kushuhudia kampuni hiyo ikiingia kandarasi ya miaka mitano (5) na klabu ya simba,mkataba huo wenye thamani ya karibu BIL 4.9 ambao mgawanyo wake ni karibu milioni 900 za kitanzania.

Mkataba huu unaweza ukawa ni moja ya mikataba bora ya udhamini kwa klabu ya simba ambayo imewahi kuingia na unauzidi hata ule wa Kampuni ya Bia ya Kilimanjaro ulomalizika mwaka jana.

Nia ya makala hii si kuuzungumzia mkataba huo kiundani kwa maana tunaamini viongozi walikuwa makini na waliwashirikisha wataalam wa mikataba ikiwemo wanasheria hadi kufikia kusainiwa kwa mkataba huu.

Dhumuni kubwa la makala hii ni kujaribu kutafakari mkataba huu na agenda kubwa iliyo mbele ya klabu ya mabadiliko ya mfumo wa kiuendeshaji,mabadiliko ambayo yanasubiri Baraka za serikali kwa maana wanachama walishakubali kimsingi kufanya mabadiliko kupitia mkutano mkuu.

Waswahili wana misemo mingi sana,moja ya misemo hiyo ni ‘maskini akipata basi matako hulia mbwata’ maana yake ni kwamba mtu aliyekuwa na njaa kwa muda mrefu akifanikiwa kidogo basi husahau shida zake na kuona ashafanikiwa,anaweza jikuta anatumia bila kujua kile alichopata anapaswa akitunze au akizalishe ili kimsaidie kwa muda mrefu zaidi.
Simba hadi kufikia mchakato wa kutaka mabadiliko ilikuwa ni sababu ya ugumu wa uendeshaji wa timu,gharama za kulipa mishahara,kusajili,kambi ya timu na gharama zingine za kiuendeshaji,simba imekuwa ikitegemea mapato ya mlangoni,udhamini wa Azam Tv,Vodacom na michango ya pesa za mifukoni kutoka kwa wadau mbalimbali wa timu hiyo,hali hii ilisababishwa kuwa katika wakati mgumu wa kushindana na matajiri wa azam au yanga ya manji kwa takriban miaka minne,hapo ndipo Mohamed dewji alipotangaza dau la kuinunua timu kwa umiliki wa hisa ambapo mchakato wake umefikia hapa ulipo,tunapenda kuwakumbusha viongozi,mkataba huu utakuwa ni sawa na mkataba wa hela ya kula tu kwa sababu utakidhi gharama za uendeshaji wa timu lakini sio kwa maendeleo mengine kama ujenzi wa uwanja,kuwa na vitega uchumi vingine,kuwa na timu imara ya vijana nk,tunaambiwa bajeti ya simba kwa mwaka inafika billion 1,kwa maana bado kutakuwa na mapungufu ya karibu milioni 200,ambazo ukiingiza udhamini wa azam tv,Vodacom na michango ya wanachama hiyo pesa itafika,lakini swali la kujiuliza,ndoto za timu kujenga uwanja wake wa mazoezi na mechi itatimia? Jibu hapana,je timu itaweza kutengeneza timu imara ya vijana kwa faida ya simba na taifa ? jibu hapana,viongozi wasilewe na huu mkataba wakaamua kufifisha juhudi za mabadiliko,simba bado inahitaji mfumo mpya wa kiuendeshaji,simba inahitaji kuajiri benchi la ufundi la maana,inahitaji kuwa na watalaam wa masoko wa maana,inahitaji kuwa na watalaam wa mambo ya rekodi na data,kuna mahitaji mengi sana ambayo tunaamini akiingia muwekezaji kuna nafasi kubwa ya kuwaweka hawa watu kwa sababu ataweza kuwalipa mishahara mizuri ili  klabu ifanikiwe,kwa mfumo huu wa sasa ambao hata kuajiri katibu mkuu wa maana au msimamizi wa mahesabu wa maana ni shida,tusitegemee kupata mafanikio.

Tunaamini Mohamed dewji kuna namna kashirikshwa kwenye huu mkataba lakini ikiwa kama hajashirikishwa itakuwa sio jambo jema,kwa mawazo yangu simba inahitaji mwekezaji zaidi kuliko hii mikataba,lakini si vibaya kuwa na hii mikataba wakati mchakato wa mabadiliko unaendelea,rai yetu,viongozi msitumie mkataba huu kusitisha hoja ya mabadiliko.

Mwisho,mwakani simba inatarajia kucheza michezo ya kimataifa(Dalili zote zipo) hivyo maandalizi yanatakiwa yaanze mapema.kuanzia usajili,kambi nk lakini ni vizuri kugawa majukumu kwa kuzikaribisha kampuni za ndege kwa ajili ya kushughulikia safari za timu itakapokuwa inasafiri,karibisheni makampuni ya vinywaji baridi kwa ajili ya maji ya wachezaji,karibisheni kampuni za bima za afya kwa ajili  ya afya za wachezaji,karibisheni hoteli au apartments kwa ajili ya kambi,zungumzeni na wamiliki wa mitandao ya kijamii ya habari kwa ajili ya kuwasaidia kutangaza mechi za simba,tangazeni tenda kwa ajili ya watu kutengeneza vifaa mbalimbali vyenye nembo ya klabu kwa makubaliano maalum(shirikisheni matawi katika hili) maana kucheza mechi ya kimataifa moja tu huwa ni fursa kubwa sana kibiashara kama klabu ikiamua kupanua wigo mpana wa kujitangaza.
Kwa kumalizia,nawapongeza viongozi kwa mkataba huu wa sportpesa lakini mabadiliko yasonge mbele.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top