SDF SPORTS SDF SPORTS Author
Title: HANSPOPE ATOA UFAFANUZI KUHUSU KUJIUZULU KWAKE
Author: SDF SPORTS
Rating 5 of 5 Des:
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspope ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii...
Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa klabu ya Simba Zacharia Hanspope ametoa ufafanuzi kuhusu taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii kuhusu kujizulu nafasi hiyo ndani ya Wekundu hao.

Leo kumekuwa na taarifa mbalimbali kutoka katika mitandao ya kijamii zinazo muhusu kiongozi huyo mwenye ushawishi mkubwa ndani ya Simba kuwa amejiuzulu.

Akizungumza na mtandao huu Hanspope amesema amejiuzulu Ujumbe wa kuteuliwa katika Kamati ya Utendaji ambapo tayari ameshaandika barua kwa Rais  Avans Aveva.

Hanspope amesema sababu zilizopelekea kujiuzulu kwake ameziandika katika barua yake na anayetaka kujua amtatufe Rais Aveva.

About Author

Advertisement

Post a Comment

 
Top